Yaliyomo
Search


Advanced Search
 

Aika Swai, New York, USA
"Sisi tunaoishi nje tunawaomba kina baba na mama, kaka na dada mumpe kura zenu Kikwete na Karume. Maisha bora kwa kila mtanzania."

 »  Home  »  Habari Mpya  »  Kikwete asema muundo wa serikali ijayo umezingatia ajenda na majukumu yaliyopo
Kikwete asema muundo wa serikali ijayo umezingatia ajenda na majukumu yaliyopo
By Mike Mushi | Published  01/5/2006 | Habari Mpya |
MUUNDO wa serikali ya awamu ya nne umetegemea ajenda na majukumu yaliyopo katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wa serikali hiyo.
 
 Rais Jakaya Kikwete alisema hayo jana alipokuwa akitangaza baraza lake la mawaziri na kuongeza licha ya majukumu na ajenda pia baraza lake limelenga katika kushirikisha uwakilishi wa jamii mbalimbali.
 
 Rais Kikwete alisema amefanyia marekebisho baadhi ya wizara kwa kuzipunguzia majukumu na kuunda wizara mpya kwa ajili ya kutekeleza ajenda zilizopo.
 
 Alisema wizara mpya aliyounda ni ya Uhusiano wa Afrika Mashariki, ambapo alifafanua kuwa mwaka jana wakuu wa nchi za Afrika Mashariki walikutana na kutaka kuanzishwa kwa wizara hiyo ili kila nchi iweze kutetea maslahi yake.
 
 Viongozi waliokutana ni Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, Rais wa Kenya, Mwai Kibaki na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, na kuamua ili nchi iweze kunufaika na isiachwe nyuma lazima kuwe na wizara itakayotetea maslahi ya kila nchi.
 
 Alisema ameamua kutenganisha Wizara ya Maji na Mifugo kwa kuwa suala la maji ni tatizo kubwa katika maeneo mengi na kila Mtanzania anayeulizwa kero yake ya kwanza, ni maji.
 
 Rais Kikwete alisema hata mifugo nayo amelazimika kuiundia wizara ya pekee kwa kuwa Tanzania ina ng'ombe milioni 17, lakini wafugaji hawafaidiki na mifugo hiyo.
 
 Alisema aliwahi kusema wakati wa kampeni kuwa kutokana na uhaba wa malisho ya ng'ombe na taabu wanayoipata wachungaji, mfugaji hanenepi na ng'ombe hanenepi.
 
 Aliongeza kuwa Wizara ya Ujenzi ameibadilisha jina na kuita Wizara ya Miundombinu kwa kuiunganisha na Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi, ili kuongeza ufanisi wake.
 
 Alisema pia katika kuangalia ajenda zilizopo mbele, ameamua kuondoa michezo, ufundi na ustawi wa jamii katika Wizara ya Kazi, Vijana na Maendeleo ya Vijana, ambapo ufundi umepelekwa kwenye Wizara ya Elimu, na Ustawi wa jamii imepelekwa Wizara ya Afya.
 
 Alisema masuala ya michezo yameunganishwa na Wizara Habari na Utamduni, kuwa chini ya wizara moja iitwayo Habari, Utamaduni na Michezo.
 
 Rais Kikwete alisema ameunda Wizara ya Usalama wa Raia ambayo itakuwa na polisi pekee yake kwa kushughulikia masuala ya uhalifu na kupambana na ujambazi unaoonekana kuota mizizi nchini.
 
 Alisema Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi sasa itashughulikia masuala ya uhamiaji, uraia, magereza na zimamoto, na suala la vitambulisho vya uraia litavaliwa njuga ikiwemo kupambana na wahamiaji haramu.
 
 Rais Kikwete alisema kuwa Wizara ya TAMISEMI imehamishiwa kutoka Ofisi ya Rais na sasa imehamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kuwa inahitaji maamuzi ya mara kwa mara.
 
 Alisema wizara aliyoiunda ya Siasa na Uhusiano wa Jamii itakuwa chini yake ili kusaidia kumaliza matatizo ya kisiasa hasa ya Pemba na Unguja, naye kama msimamizi mkuu anapenda kuwa karibu na vyama vya siasa.
 
 Hata hivyo, alisema kazi ya usajili wa vyama vya siasa itaendelea kuwa chini ya ofisi ya Waziri Mkuu na Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kazi yake itakuwa ni kusajili vyama vya siasa kama sheria inavyosema na siyo kuingilia migogoro ndani ya vyama hivyo.
 
 Rais Kikwete alisema Menejimenti ya Utumishi wa Umma itaendelea kuwa chini yake pamoja na masuala ya Utawala Bora.
 Kuhusu wizara iliyokuwa chini ya ofisi ya Makamu wa Rais iliyokuwa inashughulikia umasikini, alisema ameiondoa.
 
 Rais Kikwete alisema suala la mazingira litabaki ofisi ya Makamu wa Rais, kwa kuwa ni suala muhimu kutokana na mabadiliko ya hali ya mazingira yanavyotokea.
 
 "Tusipokuwa waangalifu, wajukuu zetu watatulaumu kwa kuharibu mazingira au kutochukua hatua madhubuti za kulinda mazingira.
 
 "Nilipokuwa Nachingwea kulikuwa na mtu mmoja ambaye kila asubuhi alikwenda na fimbo kwenye kaburi la baba yake na kuanza kulipiga huku akimlaumu kwa nini hakumsomesha, na ndiyo maana anapata taabu zote alizonazo," alisema.
 
 Rais Kikwete alisema ni muhimu kutoiharibu nchi ili wajukuu watakaokuja baadaye wasipate nafasi ya kupiga makaburi 'yetu' kutokana na shida watazozipata zitazokuwa zimesababishwa na 'sisi tuliowatangulia'.
 
 Alisema serikali mpya ina mambo mapya ambapo wengi wa mawaziri na naibu mawaziri aliowateuwa ni wapya, na kuongeza kuwa mawaziri wa zamani ambao hawakuchukuliwa, uzoefu wao utachukuliwa na siyo kwamba walishindwa kazi ila haiwezekani kurejesha baraza lote la Rais Mkapa.
 
 Akijibu maswali ya waandishi wa habari, alisema suala la kuweka picha yake katika sarafu siyo suala, na utaratibu mzuri ni ule wa kutumia picha za waasisi kwa kuwa haitowezekana kila anayeingia madarakani anaweka picha yake katika sarafu.
 
 Alisema ikiwa kila rais atakayekuja ataweka picha yake kwenye noti ama sarafu, mwishowe kutawachanganya watu.
 
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Tell us why you rated this way (optional):

Send to Author Post on Site

Comments
  • Comment #1 (Posted by an unknown user)
    Rating
    good job kikwete.
     
Submit Comment


Article Options
Popular Articles
  1. BARAZA LA MAWAZIRI
  2. Kikwete Katika Kampeni Mtwara Leo
  3. Jakaya Kikwete: Muasisi wa kasi, nguvu na ari mpya
  4. Kikwete katika kampeni Lindi
  5. Nawataka maprofesa hawa, nipeni, nitawatumia
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Mike Mushi
  2. Epson Luhwago
  3. charles nzo
  4. Eliakim T. Mwakyanjala
  5. mussa juma
No popular authors found.
 

www.ccmtz.org

Click hapa kuipa kura yako ya ndio kwa CCM.