Yaliyomo
Search


Advanced Search
 

Aika Swai, New York, USA
"Sisi tunaoishi nje tunawaomba kina baba na mama, kaka na dada mumpe kura zenu Kikwete na Karume. Maisha bora kwa kila mtanzania."

 »  Home  »  Habari Mpya  »  Jakaya Kikwete: Muasisi wa kasi, nguvu na ari mpya
Jakaya Kikwete: Muasisi wa kasi, nguvu na ari mpya
By Mike Mushi | Published  08/21/2005 | Habari Mpya |
Jakaya Kikwete: Muasisi wa kasi, nguvu na ari mpya

Na Dennis Msacky

HAKIKA Jakaya Kikwete ambaye ni mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), ni miongoni mwa wanasiasa ambao wana mvuto mkubwa kwa jamii. Mvuto huu na mengine mengi ndio uliomwezesha  kuweza kuibuka mshindi katika mchakato mgumu wenye ushindani mkali  wa kumpata mgombea urais katika chama chake.

Haiba ya Kikwete ni wanasiasa wachache sana wenye nayo. Wengi huvuma katika kipindi kifupi na baada ya hapo wanasahaulika. Wapo wanasiasa kama marehemu Oscar Kambona, Austine Lyatonga Mrema waliovuma kwa kishindo katika siasa za Tanzania, lakini kadri siku zilivyokwenda, mvuto wao kwa jamii ulishuka.

kwa Jakaya Kikwete hilo, halipo kwani kwa miaka zaidi ya kumi amekuwa kipenzi cha wanaCCM walio wengi na hata kwa Watanzania pia. Moja ya sifa  aliyonayo Kikwete  ni ile ya kuwa karibu na watu. Kushiriki katika shughuli za kijamii, nazo zimemfanya mgombea huyu awe kipenzi cha watu na hasa wajumbe wa chama hicho.

Kikwete ni mwanasiasa  asiyejiona hata pale ambako angetarajiwa kujiengua na kujiweka kwenye ngazi za ukubwa, ni mtu tofauti na wanasiasa wengine wa taifa hili.

Wengi walidhani mara baada ya kupelekwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa tangu mwaka 1995-2005, basi umaarufu wake katika siasa za ndani ya nchi ungepungua, lakini haikuwa hivyo. Nafasi hii iliweza kumpa upeo mkubwa kuhusu masuala ya nje.

Alizidi kupanda chati, ndio maana aliweza kuwaangusha vigogo wengine waliokuwa wanawania nafasi hiyo ndani ya chama. Aliibuka na ushindi mkubwa, ulioacha washindani wake hoi.

Kupanda chati katika medani ya kisiasa kwa Kikwete pia  kutokana na uwezo wake kiakili wa kujifunza mambo.Kwanza hakuna ubishi kwamba Kikwete amekomaa katika siasa, kwani alianzia katika uwanja wa Vijana akishika nyadhifa za siasa na utendaji. Kote huku aliweza kumudu vema.

Pia ni miongoni mwa mawaziri katika serikali ya sasa, waliofanya kazi katika wizara nyingi. Amefanya kazi katika wizara tatu, Nishati (Maji) na madini, Fedha na sasa mambo ya nje, pia kwa kipindi kirefu amekuwa katika Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM na baadaye Kamati Kuu ya Chama, Ana utumishi wa miaka 30 ndani ya CCM.

Kutokana na Kung'aa kwa nyota ya Kikwete kisiasa, anapewa nafasi kubwa ya kupotea kijiti kutoka kwa Rais Benjamin Mkapa, ambaye anamaliza muda wake baada ya kutumikia nchi kwa vipindi viwili vya miaka mitano mitano kwa mujibu wa katiba ya nchi.

Mkapa anamaliza kipindi chake cha miaka10 hapo Oktoba baada ya Uchaguzi Mkuu. Ushindi wa Kikwete unaonekana dhahiri kutokana naye kuwa mpenzi mkubwa wa wananchi wengi, na pia chama anagombea kupitia chama kilichodumu katika uongozi wa nchi kwa zaidi ya miaka 40. Hivyo kina mikakati imara ya kuweza kunyakua ushindi.

Hata katika mchakato mzima wa kumpata mgombea wa CCM, hakika haikuwa kazi rahisi kwani aliweza kupambana na vigogo waliokuwa wakionekana kwamba wanakubalika pia katika chama, kama vile aliyekuwa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU), Dk. Salim Ahmed Salim, waziri wa mawasiliano na uchukuzi, Pro. Mark Mwandosya. Pamoja na wagombea wengine wanane walioshika ngazi mbalimbali.

Kikwete, alizaliwa mwaka 1950, na ana shahada ya kwanza katika uchumi aliyoipata katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Katika miaka hiyo ya 1970, Kikwete angeweza kujiendeleza zaidi katika fani ya uchumi, lakini kutokana na mapenzi yake katika siasa na kuipenda TANU, aliamua kujikita zadi katika ajira ya chama, ambayo kwa madai yake ilikuwa haina kipato kizuri.

Hata hivyo, baadaye alijiunga na Jesho la Wananchi wa Watanzania (JWTZ), alikopata nyadhifa kadhaa ikiwamo ya kuwa mkuu wa masuala ya usalama katika jeshi hilo.

Hata baada ya kuingia jeshini, alirudi katika siasa na hatimaye akaingia bungeni miaka ya 80, Nyota yake iliendelea kung'ara na Mzee Ali Hassan Mwinyi alimwona akampa wadhifa za Unaibu waziri kisha waziri kamili.

Alikuwa miongoni mwa mawaziri wachache wa serikali ya awamu ya pili waliorejeshwa katika awamu ya tatu, akikabidhiwa mikopo ya Mambo ya Nje tangu mwaka 1995 hadi sasa.

Harakati zake za kutaka kuukwaa urais wa Tanzania zilianza mwaka 1995, alipoangushwa na Rais Benjamin Mkapa katika  mchakato wa kupata mgombea urais kupitia CCM. Hata hivyo, isingekuwa ni utaratibu wa ushindi wa theluthi mbili, Rais wa awamu ya tatu angekuwa ni Kikwete, Kwani katika raundi ya kwanza wakati wa kura ndani ya Mkutano Mkuu wa CCM mwaka 1995, aliongoza, mbele ya Rais Mkapa wa Waziri Mkuu wa zamani, Cleopa Msuya. Ilikuwa ni raundi ya pili iliyompambanisha Kikwete na Rais Mkapa ndiyo iliyompa ushindi Rais Mkapa.

Uhodari wake na umakini wake, hata baada ya kushindwa mwaka 1995, ulimweka Kikwete kwenye mstari safi. Aliweza kumpongeza Mkapa pale pale  Chimwaga  na kutangaza  kuvunja kundi lake na kulitakalijiunge na Mkapa kumpungia kampeni dhidi ya wagombea wa vyama vingine.

Watu wengi wanamwona Kikwete kwamba  ni mtu asiyejiona na ambaye amekulia katika misingi ya  Baba wa Taifa, Julius Nyerere. Hii ni kutokana naye kutojilimbikiza mali. Pia amekuwa mtu wa karibu na jamii na hii ndio iliyomfanya azidi kupendwa.

Tayari amekwisha kutangaza kauli miu yake: "Ari mpya, Nguvu mpya na Kasi Mpya," amekwisha kutambua kazi kubwa iliyoko mbele yake, sasa anajipanga kuitekeleza.

Katika uchaguzi wa mwaka huu, atakuwa anapambana na mgombea wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ambaye anaonekana kukua kisiasa kadri siku zinavyokwenda.

Pia atakuwa na anapambana na mgombea mwingine kutoka CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye anaonekana kuwa mvuto katika sehemu anazopita kukijenga chama chake.

kama Kikwete ataukwaa urais atakuwa na kazi moja kubwa nayo ni kuendeleza yale ambayo Mkapa ameonyesha katika uongozi wake. Mkapa ameweza kufufua uchumi wa Tanzania, ambao ulikuwa umedidimia na kuleta heshima ndani na nje ya nchi.

Gazeti-Mwananchi

ISSN-0856-75724 Tarehe Jumapili 21 Agosti 2005

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Tell us why you rated this way (optional):

Send to Author Post on Site

Comments
  • Comment #1 (Posted by an unknown user)
    Rating
    This article is focused and has very well defined the Leader and described his Vision interms of his theme:AriNguvuKasi Mpyathat seems to be motivating to many of us
     
  • Comment #2 (Posted by an unknown user)
    Rating
    The quality of this article is excellent because the author explain thourally the things which make the reader to know and vote for our new coming post of President. By : R. George
     
  • Comment #3 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Hayo yote ni kweli tupu. Huyu jamaa si mtu wa kujilimbikizia mali. Tunataka asiingiliwe na mtu yeyote anayejiona yeye ndiye BORA. Kikwetet tuchagulie waziri mkuu wa watanzania na siyo waziri mkuu wa rais. Tumechoshwa na huduma mbovu serkalini hasa zinatokana na uzembe kujuana kuajiriwa kwa ukabila nyumba ndogo na nk. Waomi wengi wanomaliza elimu ya chuo kikuu waajiriwe kuchukua nafsi nying tu makampuni ya wahindi hayaajiri watu wenye sifa YAKICHUNGUZWA NA KUBANWA NA PM YATATOA AJIRA NYINGI SAAANA. MIKATABA YA MADINI IKICHUNGUZWA TUTAWEZA KUPA ANGALAU 10 NA HII ITATOA NAFASI YA WATANZANIA KUINUA MAISHA YAKO. YEYOTE AMBAYE HAKUBALIANA NA KASI MPYA NA ARI MPYA TUNAMUOMBA AKAE MBALI!
     
  • Comment #4 (Posted by Seseyamoto Mhando)
    Rating
    SISI WANANCHI TUNATEGEMEA KATIKA ARI MPYANGUVU MPYA NA KASI MPYA JK ATAFANYIA KAZI MAKOSA YOTE YA KIBINADAMU YA RAIS MKAPA.KUONGEZA AJIRA NCHINI AFANYIE KAZI PENDEKEZO LA KUKATWA KWA MADINI YA TANZANITE HAPA NCHINI BADALA YA KUSAFIRISHWA YAKIWA GHAFI.MAKAMPUNI YA NJE YADHIBITIWE YASIAJIRI HATA WAFAGIZI WA OFISI KUTOKA INDIA AMA KENYEKIKWETE OYEE...ASANTE
     
  • Comment #5 (Posted by an unknown user)
    Rating
    ukishinda katika nafasi hii ya urais nakuomba mheshimiwa ujitahidi kuunda baraza la mawaziri ambalo litakuwa sambamba katika utendaji na uwajibikaji kwa wananchi na taifa kwa ujumla kulingana na kauli mbiu ulioitoa na si kunda baraza kwa sababu mtu alikukampenia mwita box 1219 musoma
     
  • Comment #6 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Huyu mtu Bwana hana kipingamizi anauzoefu wa kutosha. Kwani hata ukiangalia katika Mawaziri yeye hakuweza kubadilishwa wizara katika maana ya kwamba ni mtu mwadilifu mtendaji na mwenye msimamo. Kwa maana hiyo naamini atakuja na Kasi mpyaNguvu mpya pamoja Ari mpya. Lazima Kikwete ashinde kwani mtu mwenye akili timamu anayeona maendeleo yaliyofanywa na Mkapa(CCM) hawezi kukipigia kura chama cha upinzani. Na naamini watanzania tulio wengi tunaakili timamu.Kwa maana hiyo CCM Hoyeeeee Rais ni Kikwete
     
  • Comment #7 (Posted by an unknown user)
    Rating
    The story sums up the political maturity of Jakaya Kikwete as a man of strong will which is vital for leadership.his philosophy is clear that he will succeed in turning the nation into a prosperous developing state.Wish him well.
     
  • Comment #8 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Napendekeza Rais awe Kikwete na wabunge nusu wawe CCM wakuchaguliwaRobo wapinzani na waliobaki wawe viti maalumu mchanganyikoili kuleta changamoto Bungeni.
     
  • Comment #9 (Posted by an unknown user)
    Rating
    kwa kweli anastahili kuwa Rais wa nchi hii kwani ni mvumilivu na mwadilifu na mchapakazi hodari.
     
  • Comment #10 (Posted by Hellen Wilson)
    Rating
    The article has well addressed all the necessary issues that people would want to know about our new coming President. I would like to Kindly ask Mr. Kikwete to work hard on bringing back employment opertunities for Tanzanians. I dont understand how the immigration department would issue a work permit to a foreigner who has the same qualifications as a normal Tanzanian graduate. There are quite a good number of people working in Tanzania from our neighbouring countries who hold the opertunities for Tanzanians.We can not develop if we leave all the opertunities to other people and our people are suffering.
     
  • Comment #11 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Jakaya Mrisho Kikwete ni Chaguo la Watanzania tangu ulipoanza mchakato ndani ya chama cha mapinduzi Watanzania walikuwa na Imani na wewe ni Kiongozi tofauti na wengine kubwa ambalo umejijengea heshima ni kutojilimbikizia mali kitu ambacho sisi watanzania kimetupa matumaini zaidi na tuliyokuwa nayo hapo awali. Watanzania tunakutegemea wewe kwa maisha bora kwa kila mtanzania. Mungu akubariki uivushe nchi hii katika awamu hii ya nne ikiwa salama na yenye ongezeko kubwa la uchumi. MUNGU IBARIKI AFRIKA MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU MBARIKI JAKAYA KIKWETE (Rais wa nne wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania). By. JOSEPHAT MKWEMBA
     
  • Comment #12 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Mimi ni mTanzania ninaishi Denmark waTZ mpeni ushindi mgosi Kikwete sisi wengi wa TZ tunamuombea heri MR JMK Msimbazy Mwenyekiti waTanzania Denmark
     
  • Comment #13 (Posted by an unknown user)
    Rating
    cause is number one
     
  • Comment #14 (Posted by an unknown user)
    Rating
    ITS SAYIN WHAT IS NEEDED AND TRUE
     
Submit Comment


Article Options
Popular Articles
  1. BARAZA LA MAWAZIRI
  2. Kikwete Katika Kampeni Mtwara Leo
  3. Jakaya Kikwete: Muasisi wa kasi, nguvu na ari mpya
  4. Kikwete katika kampeni Lindi
  5. Nawataka maprofesa hawa, nipeni, nitawatumia
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Mike Mushi
  2. Epson Luhwago
  3. charles nzo
  4. Eliakim T. Mwakyanjala
  5. mussa juma
No popular authors found.
 

www.ccmtz.org

Click hapa kuipa kura yako ya ndio kwa CCM.