Yaliyomo
Search


Advanced Search
 

Aika Swai, New York, USA
"Sisi tunaoishi nje tunawaomba kina baba na mama, kaka na dada mumpe kura zenu Kikwete na Karume. Maisha bora kwa kila mtanzania."

 »  Home  »  Habari Mpya  »  Nawataka maprofesa hawa, nipeni, nitawatumia
Nawataka maprofesa hawa, nipeni, nitawatumia
By Mike Mushi | Published  08/30/2005 | Habari Mpya |
Nawataka maprofesa hawa, nipeni, nitawatumia

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, amewataka wapiga kura wa majimbo mawili ya Rungwe kuwachagua Profesa David Mwakyusa wa Jimbo la Mashariki na Profesa Mark Mwandosya wa Rungwe Magharibi kwa sababu anawahitaji katika utumishi.

Bila kufafanua anataka kuwatumia kwa njia gani, Mhe. Kikwete aliwasihi wapiga kura kuwachagua wagombea hao kwa sababu anawajua, ni waadilifu na wanaweza kumsaidia katika utendaji wake wa kazi.Hata hivyo, Profesa Mwandosya alipita bila kupingwa katika jimbo lake.

Akihutubia maelfu ya watu katika Kiwanja cha Michezo mjini Tukuyu, mgombea huyo alimsifia Dr. Mwakyusa kwa kusema kuwa alijitahidi sana kuokoa maisha ya mwasisi wa Tanzania, marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Hata hivyo haikuwezekana. Profesa Mwakyusa alikuwa daktari wa Mwalimu.

"Nilipokwenda kumtembelea Mwalimu kule St. Thomas Hospital, nilimkuta Dr. nakumuuliza kama inawezekana kuokoa maisha yake. Dr. Mwakyusa aliniambia kuwa 'mimi kama daktari nimemaliza. Kilichobaki ni cha Mungu. Nilimuuliza alikuwa na maana gani? Akaniambia kuwa nilivyosema ndivyo ninavyomaanisha," alisema Kikwete. Kuhusu Profesa Mwandosya, Kikwete alisema anamfahamu kwa sababu walifanya wote kazi katika Wizara moja na kisha katika serikali moja.

katika mkutano huo, Kikwete aliwatahadhalisha wananchi wa Wilaya ya Rungwe juu ya tatizo la ukimwi na kusema kuwa maambukizi katika wilaya hiyo sasa yamefikia kiwango cha asilimia 22.5

"Pamoja na kwamba serikali itaongeza kasi ya kuwapatia dawa za kupunguza makali ya ukimwi, njia nyepesi na ya uhakika ni kuwa na tahadhali katika tabia zetu," alisema mgombea huyo.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Tell us why you rated this way (optional):

Send to Author Post on Site

Comments
  • Comment #1 (Posted by an unknown user)
    Rating
    The article is excellent as it is talking about the coming president.Viva KikweteViva Shein
     
  • Comment #2 (Posted by an unknown user)
    Rating
    the way it was presented short and clear
     
  • Comment #3 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Lead(fisrt paragraph) inaelezea bayana habari unailewa mapema kabla hata hujaenda ndanihongera keep it up
     
  • Comment #4 (Posted by an unknown user)
    Rating
    inaeleza vizuri habari zake honger
     
  • Comment #5 (Posted by an unknown user)
    Rating
    It has all the that one has to say about any person qualification.
     
  • Comment #6 (Posted by Oforo Shayo)
    Rating
    This shows us how serious our expected next President HE. Jakaya Kikwete is about our Country development.
     
  • Comment #7 (Posted by Mig Joshua Oming'o)
    Rating
    Hii inaonyesha ni jinsi gani Ndugu Jakaya alivyo makini katika hotuba zake na ninauhakika akizingatia yote anayo ya sema katika hotuba zake nchi ita neemeka na kupiga hatua kubwa kimaendeleo na mpa heko na natumaini atayatekeleza anayo yasema katika kampeni zake
     
  • Comment #8 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Well articulated
     
  • Comment #9 (Posted by an unknown user)
    Rating
    what kikwete is true he needs those brains
     
  • Comment #10 (Posted by lihokola)
    Rating
    The coming presendint is comited in the development of the country that is why he needs those profesors and intelectuals
     
  • Comment #11 (Posted by an unknown user)
    Rating
    It is really very good in reporting to quote what the interviewee said it makes the whole story not yours but a reported one hence fulfilling the goal of a reporter
     
  • Comment #12 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Expected president trying to expose his focus on the deadly diseasethats good
     
  • Comment #13 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Mr. president is brilliant.
     
Submit Comment


Article Options
Popular Articles
  1. BARAZA LA MAWAZIRI
  2. Kikwete Katika Kampeni Mtwara Leo
  3. Jakaya Kikwete: Muasisi wa kasi, nguvu na ari mpya
  4. Kikwete katika kampeni Lindi
  5. Nawataka maprofesa hawa, nipeni, nitawatumia
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Mike Mushi
  2. Epson Luhwago
  3. charles nzo
  4. Eliakim T. Mwakyanjala
  5. mussa juma
No popular authors found.
 

www.ccmtz.org

Click hapa kuipa kura yako ya ndio kwa CCM.