Tanzania
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »    »  Tanzania
Tanzania
By Mike Mushi | Published  12/21/2005 | | Rating:
Tanzania Kiufupi
Nchi ya Tanzania iko katika pwani ya Mashariki ya Bara la afrika kati ya longitudo 29 na 41 Mashariki, na Kati ya latitudo l na l2 kusini. Ncha ya kaskazini kabisa ya nchi ni mji wa Bukoba, usawa wa latitudo l Kusini; na ncha ya Kusini kabisa ni mji wa Mtalika, usawa wa latitudo 12 kusini.
 
 Ncha ya Magharibi kabisa ni mji wa kigoma usawa wa longitudo 29 mashariki ya msistari wa Greenwich, na ncha ya Mashariki kabisa ni mji wa Mtwara ulioko usawa wa Longitudo 41.
 
 Kwa upande wa kaskazini, Tanzania imepakana na nchi za Kaenya na Uganda ambapo upande wa magharibi imepatana na nchi za Burundi na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Kwa upande wa kusini, Tanzania imepakana nchi za Zambia, Malawi na Msumbiji ambapo upande wa mashariki imepakana na Bahari ya Hindi.
 
 Mazingira ya Nchi:
 
 Tanzania ndiyo nchi kubw akupita nchi zote za Afrika mashariki (Kenya, Uganda na tanzania). Tanzania ina maumbile matatu ya kipekee ambayo ni Visiwa vya Zanzibar na Pemba na Ukanda wa pwani kwa upande wa mashariki, na muinuko wenye umbile la bakuli katikakakati, pamoja na nyanda za juu.

Bonde la ufa (The Greaf Rift Valley) ambalo LINAANZIA Kaskazini-Mashariki ya Bara la Afrika na kupitia katikati ya Tanzania ndiyo alama nyingine kubw inayoongeza mandhari ya nchi.

Bonde hilo la ufa limekwenda hadi kufikia kusini katika Ziwa Nyasa na kujigawa pande mbili, moja ikiendelea Kusini zaidi ya Ziwa Nyasa hadi Mozambique, na pande nyingine ikielekea Kaskazini-Magharibi pembezoni mwa Burundi, Rwanda, Tanzania na sehemu ya Magharibi ya nchi ya Uganda.
 
 Ndani ya Bonde Kuu hili la ufa, kuna msururu wa maziwa kama vile Ziwa Rukwa, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa, Ziwa Kitangiri, Ziwa Eyasi na Ziwa Manyara. Sehemu za miinuko ni pamoja na Kipengere, Udzungwa, Matogoro, Livingstone na Ufipa ambazo kwa pamoja zinafanya Nyanda za Juu za Kusini.

Safu ya milima ya Usambara, Pare, Meru, Kilimanjaro, Shimo la Volkeno la Ngorongoro na Oldonyo Lengai vyote hivi ndivyo vinavyoitwa Nyanda za Juu za Kaskazini.

Kutoka shemu hizi za miinuko pamoja na bonde la Kati ndiko kunakopita mitiririko ya maji ambayo hatimaye huishia katika bahari za Hindi, Atlantic na Mediterranean pamoja na maziwa na mabwawa yaliyomo nchini.
 
 Milima ya Tanzania:
 
 - Mlima Kilimanjaro wenye urefu juu ya usawa wa bahari wa mita 5,895
 - Mlima Meru, mita 4566
 - Mlima Rungwe, mita 2,960
 - Milima ya Uluguru, mita 2,648
 - Milima ya Rubeho, mita 2,576
 - Milima ya Livingstone, mita 2,521
 - Mlima Mbizi, mita 2,418
 - Mlima Mahari, mita 2,373
 - Milima ya Usambara, mita 2,300
Comments