JakayaKikwete.com - http://www.jakayakikwete.com/tanzania
Shein ahutubia mkutano Geneva na kutoa changamoto kwa mashirika ya kimataifa
http://www.jakayakikwete.com/tanzania/articles/520/1/Shein-ahutubia-mkutano-Geneva-na-kutoa-changamoto-kwa-mashirika-ya-kimataifa/Page1.html
By Mike Mushi
Published on 04/19/2007
 
Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein ameyapa changamoto mashirika ya kimataifa kuongeza kasi ya kuzisaidia nchi za Afrika katika kutokomeza magonjwa ambayo hayajapewa kipaumbele katika nchi za joto ili siku moja yabaki kuwa historia.

Mke wa  Rais Mama Salma Kikwete amesema uteuzi wa Dkt Asha- Rose Migiro na  Balozi Liberata Mulamula kushika nyadhifa za juu katika nyanja za kidiplomasia, kuwe changamoto kwa wanawake wengine hapa nchini kufanya vema katika shughuli zao mbalimbali.
 
Ameyasema hayo leo jioni wakati alipokuwa  akisalimiana  na  wake wa Mabalozi na  Wawakilishi wa  Taasisi za Kimataifa  hapa nchini. Mama Kikwete alikuwa ameandaa hafla fupi kwa lengo la kusalimiana, kufahamina, kubadilisha  mawazo na  uzoefu  kuhusu mambo muhimu yanayohusu  maendeleo ya wanawake na watoto.
 
“Mwaka 2006 ulikuwa mwaka muhimu kwa wanawake wa Tanzania, kwangu mimi binafsi na kwa   Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA). Katika mwaka huo   tulishuhudia wanawake wakingia katika anga za diplomasia za kimataifa. Mafanikio ya wanawake hawa ni chachu  kwa  wanawake wengine” alisema Mama Kikwete.
 
Mama Salma Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa  Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,(WAMA) alisema  uteuzi wa Migiro kuwa Naibu Katibu Mkuu wa UN na Mulamula kuwa KatibuMtendaji wa Sekretariet ya Nchi za Maziwa Makuu   kumpa shauku na  hamasa  ya kutaka kuwaona wanawake wengi zaidi wakifikia hatua za juu zaidi.
 
Aidha alisema ndio maana ameamua  kuwasaidia na kuwaendelea watoto wa kike ili nao waweze kuja kushika nyadhia za juu katika taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi.
 
Akielezea mikakati yake ya kuwasaidia watoto wa kike kupata elimu ya juu, Mama Kikwete alisema hadi sasa wanafunzi wa kike 140, kutoka Tanzania Bara na Visiwani, wamepata ufadhili wa WAMA wa kuendelea na masomo ya sekondari katika shule za Umma na za Binafsi.
 
Alisema ili kufanikisha juhudi za kumwendeleza mtoto wa kike kielimu na kuwapatia maisha bora wanawake,  ushirikiano wa karibu unahitajika kati ya taasisi yake na wake za mabalozi hao kupitia chama chao pamoja na wadau wengine.
 
Pamoja na kuelezea mikakati ya kumwendeleza mtoto wa kike kielimu, Mama Kikwete alisema taasisi yake pia imejikita katika  vita dhidi ya ukimwi mkazo ukiwa kwa vijana na mapambano dhidi ya ugonjwa wa malaria.
 
Katika hafla hiyo, Mama Salma Kikwete aliusifu mchango wa Mama Anna Mkapa kupitia  taasisi yake  ya Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) kwa namna alivyochangia kusukuma mbele maendeleo ya wanawake na watoto hapa nchini.
 
Alisema kuwa kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Mama Mkapa, ndiyo iliyomsukuma na yeye kuendeleza kazi hiyo ya kuwasadia wanawake na watoto wa Tanzania  kwa kuanzisha WAMA ili wapate maisha bora.
 
Akizungumza kwa niaba  ya wake za mabalozi hao, Mke wa Balozi wa Sweden, alimshukuru Mama Salma Kikwete kwa kuwakutanisha pamoja  na wakampongeza kwa jitihada anazofanya za kuwaendeleza wanawake na watoto hapa nchini.
 
Wake hao wa mabalozi wameahidi kumpa ushirikiano wa hali na mali ili aweze kutekeleza majukumu aliyojipangia.