Hatukubali Pwani ibaki nyuma – Lowassa
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Hatukubali Pwani ibaki nyuma – Lowassa
Hatukubali Pwani ibaki nyuma – Lowassa
By Mike Mushi | Published  05/9/2007 | Habari Mpya | Rating:
· Halmashauri zikae ndani ya mwezi mmoja kupanga mikakati


 Lazima watu wafanyekazi hata ikibidi kutumia sheria ndogo
 Maisha Bora kwa Kila Mtanzania ni pamoja na mkoa wa Pwani

WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amesema kuwa haikubaliki mkoa wa Pwani uendelee kubaki nyuma kiuchumi na kimaendeleo nchini na kwamba bidii ya kufanya kazi na kilimo cha kisasa kitumike kubadili hali hiyo.

Alikuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara eneo la Kiparang’anda wilaya ya Mkuranga katika siku yake ya pili leo (Jumapili Mei 6, 2007) ya ziara ya siku sita ya mkoa wa Pwani.

Waziri Mkuu ambaye ofisi yake ndiyo inayosimamia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa aliagiza kuwa ndani ya mwezi mmoja Halmashauri zote za Wilaya za mkoa wa Pwani zikutane na kupanga mikakati ya kuondoa umasikini Pwani.

“Baadaye ya kupanga mikakati yenu wote viongozi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa tutakutana kuona tunakwenda vipi…Lazima tuibadili hali hii,” aliongeza.

Katika mkutano wake wa hadhara wa leo, Waziri Mkuu Lowassa alirudia alichokisema jana (Jumamosi Mei 5, 2007) Kibaha alipoanza ziara hii kuhusu umasikini katika mkoa wa Pwani.

Leo (Jumapili Mei 6) na jana (Jumamosi Mei 5) alitoa mfano wa pato la mwaka la kila mtu ambalo kwa Pwani bado liko chini kwa kulinganisha na mikoa jirani yenye mazingira yanayofanana na Pwani. Pato la mwaka la kila mtu Pwani ni Sh. 268,944; Lindi Sh. 315,328; Morogoro Sh. 375,647 na Tanga Sh. 439,576.

“Pwani bado mko nyuma kiuchumi na kimaendeleo…Tumieni ardhi kubadili hali hii. Ikiwezekana inabidi kutunga hata sheria ndogo ili kuwalazimisha watu wafanye kazi” aliongeza katika mkutano wa Kiparanganda.

Waziri Mkuu Lowassa pia alikemea tabia ya kuwatia mamba wasichana wa shule na kuwakatisha masomo yao. Alichukizwa alipoambiwa kuwa mwaka jana wasichana 42 waliokuwa shuleni walitiwa mimba na mwaka huu tayari 10.

Aliwataka viongozi wampe taarifa ni hatua gani za kisheria zimechukuliwa kwa waliobainika kuwa wamewatia mimba wasichana wa shule pamoja na wazazi wa wasichana hao walioficha kutoa habari hizo.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliwataka wananchi wa mkoa wa Pwani watekeleze kuanzia Julai mwaka huu agizo la Rais Kikwete kuwa kila kijiji kijenge zahanati na kila kata iwe na kituo cha afya nchini kote.

Kabla ya mkutano wa hadhara, Waziri Mkuu alipata taarifa ya Wilaya ya Mkuranga, alifungua SACCOS ya walimu katika Chuo cha Ualimu Vikindu, alitembelea shule mpya za sekondari za Vikindu na Kiparang’anda na kuona shamba la mfano la mikorosho ya mbegu mpya la mstaafu wa jeshi, Yahya Athumani Kipira.

Katika mkutano huo, Waziri Mkuu pia alipokea hundi ya Sh. Milioni 64 kutoka kampuni ya uchimbaji gesi ya Songas kwa ajili ya ujenzi wa sekondari Jambani (Sh. Milioni 49.3) na nyumba ya walimu katika shule ya msingi ya Njopeka (Sh. Milioni 14.9). Pia alipokea mabati 500 kutoka kwa mfadhili Bw.Mutembei, ambaye ni mmiliki wa shule ya Sekondari ya St. Mathey iliyopo Kongoe.

Waziri Mkuu ambaye alisema alivutiwa na ujenzi wa shule ya sekondari ya Kiparang’anda alitoa Sh. Milioni 1 kwa ajili ya maendeleo ya shule na mipira miwili, mmoja kwa wavulana na mwingine kwa wasichana, kwa ajili ya kucheza.

Jana (Jumamosi Mei 5, 2007) akiwa katika wilaya ya Kibaha, Waziri Mkuu alizindua kiwanda cha kubangulia korosho cha Michael Lund Cashewnut Processing Centre ambacho ni cha kikundi cha ushirika cha Uvuki katika eneo la Visiga.

Alisifu kikundi cha Uvuki kwa kubuni ushirika huo na kuongeza thamani ya korosho kwa kuibangua kiwandani na kutaka maeneo mengine yanayolima korosho yaige mafanikio ya kikundi hicho.

Mapema alitembelea kituo cha utafiti wa kilimo kilichopo Tumbi, Kibaha na kuweka jiwe la msingi la sekondari ya Mwanalugali kabla ya kukagua shughuli za SACCOS za kikundi cha Mlandizi.

Kesho (Jumatatu Mei 7, 2007) atatembelea wilaya ya Rufiji. Wilaya nyingine atakazotembelea ni Mafia, Kisarawe na Bagamoyo kukamilisha ziara ya mkoa wa Pwani.
(mwisho)

 
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments