Wakurugenzi zaidi wa mamlaka za Serikali za Mitaa wahamishwa.
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Wakurugenzi zaidi wa mamlaka za Serikali za Mitaa wahamishwa.
Wakurugenzi zaidi wa mamlaka za Serikali za Mitaa wahamishwa.
By Saidi Nguba | Published  07/30/2007 | Habari Mpya | Rating:
MAJINA zaidi ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa waliohamishwa kutokana na kuanzishwa Halmashauri za Wilaya mpya na kuteuliwa kwa Wakurugenzi wapya hivi karibuni yatajwa.
 
 Waliopata uhamisho na vituo vyao vya kazi vya zamani katika mabano ni Theones A. Nyamhanga anayekwenda Babati (akitokea Musoma); Gladys Dyamvunye, Ileje (Mpwapwa) na Halifa H. Hida, Arusha (Mufindi).
 
 Wengine ni L.A. Shimwela, Mufindi (Kishapu); Andrew F. Juma, Meatu (Kiteto); Jacob Kayange, Rorya (Tarime); Yona Mlaki, Mpwapwa (Ileje) na Frederick Ntabakanyule, Musoma (Handeni).
 
 Uhamisho huo unatokana na kuanzishwa kwa Halmashauri za Wilaya mpya nane na kubadilisha majina nyingine mbili na kupandisha hadhi Mamlaka za Miji Midogo ya Mpanda na Njombe kuwa Halmashauri za Mji.
 
 Halmashauri mpya ni Arusha, Longido, Bahi, Misenyi, Chato, Nanyumbu, Mkinga na Rorya.
 
 Kutokana na kuanzishwa kwa Halmashauri hizo mpya, kubadilisha majina nyingine mbili na kupandisha hadhi Mpanda na Njombe kuwa Halmashauri za Miji, Waziri Mkuu Edward Lowassa aliwateua Wakurugenzi wapya wa Mamlaka za Serikali za Mitaa.
 
 Wakurugenzi wapya waliotangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na vituo vyao vya kazi ni Christian M. Laizer, Longido; Elly Jesse Mlaki, Kishapu; Fortnatus Fwema, Iramba; Hamida Kikwega, Chato na Lucy L. Msofe, Lushoto.
 
 Wengine ni Shaibu Mnunduma, Bukoba; Festo L. Kang’ombe, Kiteto; Mohammed S. Nkya, Nanyumbu; Mariam Mtunguja, Nachingwea; Beatrice Msomisi, Bahi na Xavier Tilweselekwa.
 
 Wakurugenzi waliohamishwa na kutangazwa mwishoni mwa wiki iliyopita na vituo vyao vya zamani kwenye mabano ni Dk. Isdor Mtalo, Misenyi (Iramba); Philibert Ngaponda, Mkinga (Babati); na Tarsias B. Kagezi, Tarime (Nachingwea).
 
 Katika mabadiliko hayo, Mohammed Gwalima ameteuliwa kuwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino.
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments