Wazazo acheni kuwalinda wanaowapa mimba wanafunzi.
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Wazazo acheni kuwalinda wanaowapa mimba wanafunzi.
Wazazo acheni kuwalinda wanaowapa mimba wanafunzi.
By Freddy Maro | Published  07/31/2007 | Habari Mpya | Unrated

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amekemea vikali tabia ya baadhi ya wazazi kuwalinda watu wanaowapa mimba wanafunzi mkoani Lindi na kusema kuwa tabia hiyo ina zorotesha juhudi za serikali kumwendeleza kielimu mtoto wa kike.

Mama Salma aliyasema hayo wakati ya hafla fupi ya kugawa vitabu katika shule mbili za msingi za Chikonji na Kinengéne zote za mkoani Lindi jana alipozitembelea shule hizo kukagua maendelo ya elimu na kuzungumza na waalimu pamoja na wanafunzi.

“Ni jambo la kusikitisha kuona mzazi anashiriki katika kumtetea mtu aliyempa ujauzito mtoto wake baada ya kurubuniwa kwa fedha kidogo.Kufanya hivyo ni kumharibia maisha mtoto wa kike na kumwacha atumbukie katika lindi la dhiki na umaskini,” alisema.

Mama Kikwete aliendelea kusema kuwa mtoto wa kike anastihili kuendelezwa kielimu sawa sawa na mtoto wa kiume ili kumwezesha kutoa mchango wake wa maendeleo katika jamii akionya kuwa mimba za utotoni ni kikwazo kikubwa kwa maendeleo ya mtoto wa kike.

Aliendelea kuonya kuwa wanafunzi wa shule za msingi kupata ujauzito siyo tu unamkosesha mtoto wa kike fursa ya kujiendeleza kielimu bali pia unamweka katika hatari ya kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa kufanya ngono isiyo salama.

Akizungumza katika hafla hiyo, mkuu wa mkoa Lindi Mheshimiwa Said Sadik aliwahimiza waalimu kutafuta nyumba karibu na maeneo ya shule wanazofundisha wakati mamlaka husika ikijipanga kuwajengea nyumba katika maeneo ya shule.

Vile vile mkuu huyo wa Mkoa ametoa amri kwa watu walovamia na kujenga katika maeneo ya shule kuhama mara moja ili kuruhusu upanuzi wa shule hizo ili watoto wengi zaidi mkoani Lindi wapate fursa ya kupata elimu.

Wakisoma risala zao mbele ya mgeni Rasmi, waalimu wa kuu wa shule hizo mbili wamesema kuwa ukosefu wa maji,upungufu wa vitabu na madarasa pamoja na ukosefu wa nyumba za waalimu ni kati ya matatizo sugu yanazozikabili shule hizo mbili.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments