Lowassa kuanza ziara ya Mara kesho
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Lowassa kuanza ziara ya Mara kesho
Lowassa kuanza ziara ya Mara kesho
By Irene K. Bwire | Published  08/26/2007 | Habari Mpya | Unrated
WAZIRI MKUU Edward Lowassa kesho (Jumatatu, Agosti 27, 2007) anatarajiwa kuanza ziara ya siku sita katika Mkoa wa Mara ambako atakagua shughuli za maendeleo.
 
 Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Waziri Mkuu anatarajiwa kuwasili mkoani humo kesho asubuhi na mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Musoma, atakwenda Ikulu Ndogo na kisha atakwenda katika Ukumbi wa Uwekezaji ambako atapokea Taarifa ya Mkoa na Wilaya ya Musoma.
 
 Baada ya kupokea taarifa hizo, Waziri Mkuu atakwenda Kiwanda cha Samaki cha Prime Catch ambako atapokea taarifa ya kiwanda hicho na baadaye atazuru Chuo cha Veta ambako atapanda mti wa kumbukumbu.
 
 Kwa mujibu wa ratiba hiyo, baadaye mchana atakagua kiwanda cha Musoma Diary na kupokea taarifa ya kiwanda, na baadaye atakwenda hospitali ya Kwangwa atakokagua majengo ya hospitali hiyo.
 
 Waziri Mkuu baada ya kutoka hospitali ya Kangwa atakwenda Uwanja wa Karume ambako atakuwa na mkutano wa hadhara kuanzia saa 10 jioni. Jumanne asubuhi, Waziri Mkuu atakwenda Mugango ambako atapata taarifa fupi ya mradi wa kilimo cha umwagiliaji na matumizi ya wanyamakazi; nyati na ng’ombe.
 
 Baada ya kutoka Mugango atakwenda Bwai Kumsoma ambako atakagua na kupata taarifa ya Mwalo wa kupokelea samaki na kuzindua mwalo huo. Anatarajiwa baadaye kwenda Gereza la Kiabakari ambako atapokea taarifa fupi ya shamba la mbegu kinzani za muhogo na kukagua mbegu hizo.
 
 Kwa mujibu wa taarifa hiyo, kutoka Kiabakari, Waziri Mkuu atakwenda Sekondari ya Chifu Ihunyo ambako atapokea taarifa fupi, kukagua shule na ataweka jiwe la msingi la Ukumbi wa Lowassa. Baadaye atakwenda Nyamisisi ambako atafanya mkutano wa hadhara.
 
 Kwa mujibu wa ratiba hiyo, Jumatano atakwenda Shule ya Sekondari ya Kabasa, wilayani Bunda. Huko atapokea Taarifa ya Wilaya, Taarifa ya Sekondari na ataweka jiwe la msingi kwenye nyumba ya mwalimu na kufungua kisima cha maji. Waziri Mkuu pia atazuru Chuo cha Ualimu Bunda ambako atazindua kituo cha mawasiliano (internet) na kisha atakwenda Guta. Baadaye atazuru Bulamba Gineri ambako atazindua mashine mpya za Gineri na kuhutubia mkutano wa hadhara.
 
 Kutoka Bunda Waziri Mkuu atakwenda Wilaya ya Serengeti ambako atakagua eneo jipya la kiwanja cha ndege cha Mugumu, kukagua ujenzi wa Bwawa la Manchira na kukabidhi hundi kwa Vijana Saccos kabla ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mbuzi.
 
 Akiwa wilayani Tarime Ijumaa, Waziri Mkuu atakagua kituo cha mafunzo ya wakulima na kuweka jiwe la msingi katika chuo cha wauguzi na kuhutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Sabasaba.
 
 Atafanya majumuisho Jumamosi asubuhi mjini Musoma kabla hajaondoka kuelekea Arusha.
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments