Shein aagana na Balozi wa China
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Shein aagana na Balozi wa China
Shein aagana na Balozi wa China
By Penzi Nyamungumi | Published  09/27/2007 | Habari Mpya | Rating:
Kuongezeka kwa safari za kibiashara kati ya China na Tanzania kumeelezwa kuwa ni hatua muhimu katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi mbili hizo
 
 Balozi wa China anayemaliza muda nchini bwana Yu Qintai amesema katika miaka ya hivi karibuni uhusiano wa kibiashara kati ya nchi yake na Tanzania umekuwa ukiimarika kwa kasi na hii inadhihirishwa kwa kuwepo kwa ongezeko kubwa la safari za kibiashara kati ya nchi yake na Tanzania.
 
 Alifafanua kuwa serikali ya nchi yake inaipa umuhimu mkubwa sekta binafsi hivyo ushirikiano kati ya sekta kama hiyo nchini Tanzania ni muhimu katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.
 
 Balozi Qintai alikuwa akizungumza na Makamu wa Rais Dk Ali Mohammed Shein aliyemtembelea Ofisini kwake Ikulu kwa ajili ya kumuaga baada ya kumaliza kipindi chake cha kazi humu nchini.
 
 Balozi huyo alieleza kufurahishwa kwake na namna serikali na wananchi wa Tanzania wanavyokabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo mageuzi ya kichumi na kijamii huku ikimarisha utulivu wake wa kisiasa na kijamii.
 
 Katika mazungumzo hayo Makamu wa Rais alimpongeza na kumshukuru Balozi Yu Qintai kwa jitihada zake binafsi alizochukua katika kuimarisha uhusiano kati ya nchi yake na Tanzania wakati wote alipokuwa nchini.
 
 ‘wakati wa kipindi chako cha kazi tumeshuhudia jitihada zako binafsi katika kubuni maeneo mpya ya uhusiano na ushirikiano na kushughulikia utekelezaji wa makubaliano tuliyofikia kwa nyakati mbalimbali’ alifafanua.
 
 Dk Shein alimueleza Balozi huyo kuwa pamoja na ukweli kuwa mafanikio ambayo Tanzania imekuwa ikiyapata katika nyanja mbali mbali yanatokana na jitihada za watanzania wenyewe lakini pia misaada ya nchi rafiki kama China imekuwa chachu ya mafanikio hayo.
 
 Makamu wa Rais alisisitiza umuhimu wa ushirikishwaji zaidi wa sekta binafsi za nchi mbili hizo ikiwa ni njia mojawapo ya kuvutia mitaji na kuongeza uwekezaji nchini.
 
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments