|
Rais Jakaya Kikwete amezitaka Wizara za Maendeleo ya Mifugo na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kuhakikisha kwamba wanafunzi 86 wanaomaliza mafunzo yao katika Chuo cha Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Mifugo wanapata ajira serikalini. Ametoa agizo hilo leo wakati alipoitembelea Taasisi hiyo ya Taifa ya Utafiti wa Mifugo iliyopo Wilayani Mpwapwa, Mkoani Dodoma kukagua shughuli za Taasisi hiyo ambayo pia inatoa mafunzo ya ngazi ya diploma na cheti katika maeneo ya tiba za mifugo na uzalishaji wa mfungo. Mkuu wa Chuo hicho ambacho kilianzishwa mwaka 1935 , Dkt. Jerome Bahami , alimweleza Rais kwamba, kwa mwaka huu chuo hicho kina wanafunzi 86 wa mwaka wa pili na wa mwisho, na robo tatu yao wakiwa wanajilipia wenyewe, na kwamba wengi wao hawana uhakika wa ajira baada ya kumaliza masomo yao. “ kwanini hawa wakose ajira wakati tunauhaba mkubwa wa wataalam” akahoji Rais na Kuendelea . “huku tunasema tunatakakufanya mageuzi katika kilimo na ufugaji, hivi kinachokwamisha hawa wasijariwe ni nini, hata kama wamelipiwa na wazazi wao, lakini mzazi anapomlipia mwanae matumaini yake si apate ajira baada ya kumaliza masomo yao. Fanyeni utaratibu wa kuwaajili hawa” akasema Rais huku akimwelekea Naibu Waziri wa Mifugo, Dkt Charles Mlingwa. Pamoja na kuangiza wizara husika kuwaajiri wahitimu hao, Rais pia ameshauri kufanyiwa marekebisho au kufutwa kabisa kwa Sheria Namba Nane. Amesema Sheria hiyo ni kikwazo katika utoaji wa ajiri hasa kwa wataalamu wa kada maalum ambao mahitaji yao ni makubwa lakini ni wachache. “ Nchi inashida kubwa ya wataalamu , leo hii kwa mfano wizara au halmashauri inatangaza nafasi za wataalamu wa mifugo, na wataalamu hao wako 10, halafu mnasema ni lazima wahojiwe na madiwani, madiwani wenye elimu yao ni ya chini kuliko wataalamu hao, hivi jamani tunakwenda wapi, sheria hii ifanyiwe marekebisho ni ucheleweshaji wa muda tu na kuwapa watu posho” akasema Rais. Ameongeza kwamba zinapojitokeza nafasi za ajira kwa kada maalum, badala ya kuzitangaza nafasi hizo magazeti, wahusika waende moja kwa moja vyuoni na kuwatambua watu wanaowataka, na wakimaliza masomo yao na kutithibishwa na vyuo vyao kwamba wamefaulu vizuri basi waajiriwe. “Haiwezekani, wataalamu mbalimbali wakakosa ajira serikalini, kwa vile tu eti sheria namba nane inataka kila nafasi ya ajira itangazwe kwa sababu tu wakubwa fulani wamesema huu ndio utaratibu wa uwazi, hapana lazima tufikie mahali maamuzi mengi tuyabadilishe tu” akasisitiza Rais Chuo hicho cha Taasisi ya Utafiti wa Mifugo mwaka huu kinatarajiwa kuchukua wanafuzi 210 ambao watalipiwa na serikali kwa asilimia 100 na baada ya kumaliza masomo yao wataajiliwa na serikali. Akiwa kwenye taasisi hiyo, Rais Kikwete alitembelea mashamba ya mifugo na kujionea ng’ombe aina ya Mpwapwa wanaozalishwa katika taasisi hiyo, pamoja na mbuzi aina ya Malya ambao nao huzalishwa hapo. Rais aliwataka wataalamu hao, kuongeza kasi ya uzalishaji wa madume ya kisasa kwa kutumia teknolojia ya chupa, kwa lengo la kupata madume mengi ya kisasa ili kubadili aina ya ng’mbe waliopo ambao hawazalishi nyama ya kutosha, maziwa na hata ngozi bora. Akasema serikali itakafanya kila lilo ndani ya uwezo wake, kuisaidia Taasisi hiyo na chuo cheke ambavyo amesema ni muhimu sana katika utekelezaji wa mageuzi ya sekta ya mifugo nchini. Awali Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, Dkt Regnald Mbwile, amemweleza Rais kwamba Taasisi hiyo ambayo ilianzishwa mwaka 1905 na Wajerumani. Wakati huo ikiwa kama kliniki ya kutibu magonjwa ya mifugo. Amefafanua kwamba, Tasisi hiyo ambayo ina josho la kuoshea mifugo ilikiwa ni la kwanza Afrika mashariki lilijengwa mwaka 1905 na hadi leo hii linafanya kazi, pia kuna vituo vya utafiti wa mifugo vitafu ambavyo ni vya mabuki kiliochopo kanda ya Zuwa, kituo cha Utafiti wa Mifugo Uyole kilichopo kanda ya Nyanda za Juu kusini na kituo cha utafiti wa malisho Kongwa. Aidha ameyaeleza malengo ya Taasisi ni kuchangia katika kujitosheleza kwa chakula na maendeleo ya kiuchumi kwa kufanya tafiti sahihi na endelevu ambazo zinalenga kuongeza tija katika mifugo kwenye kanda mbalimbali za kilimo nchini. Akieleza zaidi shughuli za Taasisi hiyo, Dkt. Mbwile amesema, taasisi inaendeleza uzalishaji wa ng’ombe wa aina ya Mpwapwa ambao ni chotara kwa ajili ya nyama na maziwa, ambapo ng’ombe mmoja huweza kutoa hadi lita tisa za maziwa kwa siku na kilo 230 za nyama. “Mhe. Rais shughuli zenu nyingine ni uendelezaji na uzalishaji wa mbuzi wa aina ya Malya au Blended Goat kwa ajili ya nyama na maziwa, kuchagua na kukoosafu mifugo ya asili, kushirikiana na wadau wengine wanaojishughulisha na uendelezaji wa mifugo na uzalishaji na usambazaji wa mfugo yenye tija vijijini” akasema Dkt Mbwile. Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Mifungo pia hujishughulisha na kufanya tathimini na kuboresha vyakula vya mifugo, kutathimini na uboreshaji wa malisho na nyanda za malisho, utoaji wa habari kuhusu teknolojia zilizopo na kufanya tafiti zinazohusu masuala mtambuka kama vile mtizamo wa jinsia, athari za ukwimi, matumizi ya ujuzi asilia na hifadhi ya mazingira.
|