Serikali kunusuru mahindi Ruvuma - Lowassa
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Serikali kunusuru mahindi Ruvuma - Lowassa
Serikali kunusuru mahindi Ruvuma - Lowassa
By Saidi Nguba | Published  09/7/2007 | Habari Mpya | Unrated
WAZIRI Mkuu Edward Lowassa amesema serikali inakusudia kuyanusuru mahindi ambayo yamekosa soko katika mkoa wa Ruvuma kwa kuyanunua kupitia Kitengo cha Akiba ya Chakula cha Taifa (SGR).
 
 Kutokana na wingi huo wa mahindi, wafanyabiashara wamekuwa wakinunua mahindi kutoka kwa wakulima kwa bei ya kutupa ya sh. 50 kwa kilo moja au chini ya bei hiyo hali ambayo wananchi wamemlalamikia Lowassa kwamba ni unyonyaji.
 
 Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Msindo, baada ya kufungua shule ya sekondari katika kijiji hicho wilayani Namtumbo, Ruvuma, Waziri Mkuu alisema kwa sasa sheria inaruhusu SGR kununua mazao yale yanayobaki sokoni baada ya wafanyabiashara kutosheka hali ambayo haimsaidii sana mkulima, hivyo serikali iko mbioni kuunda shirika ambalo litakuwa linanunua nafaka.
 
 Waziri Mkuu alisema kwamba SGR itanunua mahindi hayo kwa sh. 180 kwa kilo moja na alionyesha kusikitishwa kwake kwa namna wafanyabiashara wanavyowanyonya wakulima na kusisitiza kuwa vyama vya ushirika ndiyo nguvu ya wakulima.
 
 Alisema uamuzi huo umechukuliwa kutokana na taarifa ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, bibi monica mbega ambaye alisema kwamba, mkoa una ziada ya tani 100,000 za mahindi na kiwango cha tani 4,500 tu kilichopangwa kununuliwa na SGR ni kidogo na kutaka angalau zinunuliwe tani 27,000.
 
 Waziri Mkuu Lowassa alisema kwamba, walimshauri Rais Jakaya Kikwete kuhusiana na tatizo hilo naye akaafiki na ikaamuliwa kwamba SGR haitanunua mahindi katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Shinyanga na badala yake fedha zilizotengwa kwa ajili ya mikoa hiyo zitatumika kununulia mahindi katika mkoa wa Ruvuma, Rukwa na Iringa.
 
 “Sumbawanga watanunua tani 7,000, Makambako tani 6,000 na Songea tani 14,500. Tumetoa fedha katika mikoa hiyo mitatu kwa sababu inaweza kupata soko Dar es Salaam, Kibaigwa na hata Rwanda au Burundi kwa urahisi kuliko huku Songea ambako wafanyabiashara hawawezi kuja kwa urahisi,” alisema.
 
 Alisema serikali ya Chama Cha Mapinduzi imedhamiria kwa dhati kuboresha maisha ya Watanzania ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mazao ya wakulima yananunuliwa kwa bei nzuri.
 
 Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Lowassa amesema kwa sababu sheria inaruhusu SGR kununua mazao yale yanayobaki sokoni baada ya wafanyabiashara kutosheka hali ambayo haimsaidii sana mkulima, hivyo serikali iko mbioni kuunda shirika ambalo litakuwa linanunua nafaka.
 
 “Kazi ya SGR ni ununuzi wa mazao yaliyobaki sokoni…serikali inaangalia uwezekano wa kutunga sheria itakayounda shirika la kushughulikia ununuzi na uuzaji wa nafaka (NationalGrains Board) katika mwaka mmoja ujao,” alisema Waziri Mkuu Lowassa huku akishangiliwa.
 
 Wakati huohuo, akiwa katika Kituo cha Watawa wa Benedictine wa Afrika katika kijiji cha Hanga, mara baada ya kuweka jiwe la msingi la hosteli ya kituo hicho, Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi waliohudhuria uzinduzi huo kwamba serikali ina akiba ta tani 122,000 na kwa kuanzia itauza tani 22,000 za mahindi ili kupata kiasi cha sh. bilioni 4.5 ambazo pia zitatumika kuongezea fedha za ununuzi wa mahindi ya wakulima katika mikoa itayakuwa na ziada ya nafaka.
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments