Taarifa ya Ziara ya Rais Lindi - Kilwa
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Taarifa ya Ziara ya Rais Lindi - Kilwa
Taarifa ya Ziara ya Rais Lindi - Kilwa
By Ikulu Press | Published  11/19/2007 | Habari Mpya | Unrated
 Serikali ya Awamu ya Nne inaendelea kutekeleza ahadi zake iliyozitoa wakati wa kampeni za Urais kama ilivyoainishwa na Ilani ya Chama Cha Mapinduzi.
 
 “Tuliahidi kufanya jitihada za kuinua huduma bora za kiuchumi na kijamii ili kuinua hali ya maisha ya Watanzania na kuongeza kipato cha mwananchi” Rais Kikwete amewaambia wananchi wa Somanga wakati wa kukabidhi vifaa mbalimbali kwa wananchi wa Somanga vitakavyowasaidia katika shughuli zao za uvuvi.
 
 Jumla ya shilingi milioni 125 zimetengwa kwa ajili ya kuvisaidia vikundi mbalimbali katika wilaya za Kilwa, Mafia na Rufiji.
 
 Rais Kikwete pia ameweka jiwe la msingi katika kituo cha umeme wa gesi asilia cha Somanga, ambacho ni moja ya kilio cha wananchi wa Kilwa wakati wa kampeni.
 
 Rais aliahidi huduma hiyo na sasa imeshafikia hatua ya awali ambapo huduma ya umeme inatarajiwa kuanza mapema mwaka ujao.
 
 “Tumetimiza ahadi, na tunasema tunatenda na tutatenda yote tuliyoahidi wananchi zikiwemo huduma za afya, elimu, maji, umeme na kuongeza tija katika shughuli mbalimbali za kilimo na kiuchumi” amesema.
 
 Kituo cha Umeme cha Somanga kitanufaisha wananchi wapatao 3500 katika vijiji mbalimbali wilayani Kilwa na mara kitakapokamilika kitakabidhiwa kwa Shirika la Umeme la Tanzania (TANESCO) ili kukiendesha.
 
 Katika huduma za jamii, Wilaya ya Kilwa imepiga hatua katika ujenzi wa shule za sekondari kwa kutimiza lengo la kila kata kuwa na shule ya sekondari na kupeleka watoto shule kwa asilimia 96.
 
 Wilaya ya Kilwa pia inakabiliwa na uhaba wa maji salama kwa matumizi ya binadamu na kufikia Julai 2007, Serikali ilishatenga shilingi milion 404.6 kwa ajili ya kufanyia ukarabati mabomba na visima mbalimbali katika vijiji 58 wilayani humu.
 
 Katika bajeti ya mwaka huu, Serikali pia imetenga shilingi bilioni 1.48 kwa ajili ya huduma mpya ya maji kwa vijiji 10 na inatarajiwa kuwa ifikapo mwanzo wa mwaka ujao, visima vipatavyo vitano vitaanza kutoa huduma hiyo kwa wananchi.
 
 Rais Kikwete pia ameeleza azma ya Serikali kuhakikisha barabara ya Kilwa-Mbwemkulu-Mingoyo kuwa kazi inaendelea vizuri na kukamilika mapema iwezekanavyo na kwamba kipande kilichobaki cha Somanga-Darajani, chenye urefu wa km, 60 kinafanyiwa utaratibu wa kupatiwa mkandarasi na kwamba matatizo yaliyopo kwa sasa yatatatuliwa kama ilivyopangwa.
 
 Rais Kikwete leo anaendelea na ziara wilayani Liwale ambapo anatarajiwa kufungua daraja la Mto Ruhuhu.
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments