Barabara kuu iendayo mikoa ya kusini yakamilika
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Barabara kuu iendayo mikoa ya kusini yakamilika
Barabara kuu iendayo mikoa ya kusini yakamilika
By Premi Kibanga | Published  11/19/2007 | Habari Mpya | Rating:
 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo amekagua barabara kuu ya Dar-Kibiti-Lindi hadi Mingoyo na Masasi-Mangaka yenye urefu wa Km 480.8 pamoja na Daraja la Umoja inayotarajiwa kukamilika mwezi ujao.

“Tuliwaahidi wakati wa kampeni kuwa mkituchagua barabara hii tutaikamilisha na sasa imekamilika” Rais amewaambia wananchi katika sehemu mbalimbali akiwa njiani kuelekea kutoka Lindi kwenda Kilwa kabla hajarejea Dar-es-Salaam baada ya kukamilisha ziara yake mkoani Lindi. “Na tutaendelea kuwatumikia na hatimaye kutimiza ahadi zote kama tulivyoahidi, nawahakikishia kazi tumeshaianza na inaendelea vizuri,” Rais amesema.

Barabara hii imekuwa kero kwa wananchi wa mikoa ya kusini kwa miaka mingi tangu 1995 hadi kusababisha malalamiko toka kwa wananchi kuwa wamesahaulika, hivyo kukamilika kwake kutaondoa adha na kuchochea maendeleo katika mikoa ya kusini ambayo ina hazina kubwa katika kuleta maendeleo Tanzania.

Serikali imedhamiria kutumia pesa nyingi katika kutengeneza miundo mbinu na huduma za kijamii kwa ujumla kama shule, hospitali na pia kuchangia katika shughuli mbalimbali za kiuchumi za wananchi wake na kuboresha maisha yao

Ujenzi wa barabara hii uko kwa awamu ambapo hadi sasa Km. 129 za barabara kati ya Dar-Kibiti zimekamilika kwa kiwango cha lami na Km. 4 zilizobaki zinatarajiwa kukamilika mwezi ujao na kugharimu shilingi bilioni 15.

Barabara ya Ndundu-Somanga yenye urefu wa Km. 60 inatafutiwa mkandarasi ili kuanza matengenezo chini ya udhamini wa Kuwait Fund, OPEC na Serikali ya Tanzania.

Barabara ya Nangurukuru-Mbwemkuru yenye Km. 95 inatarajiwa kugharimu shilingi bilioni 39.2 na inatarajiwa kukamilika mapema mwaka ujao. Km. zipatazo 78 zimekamilika kwa kiwango cha lami na ujenzi umefikia asilimia 93.


Barabara ya Mbwemkuru-Lindi-Mingoyo yenye urefu wa Km. 95 ina thamani ya shilingi bilioni 51.5 nayo imeshakamilika kwa asilimia 94 kwa ikiwa ni Km. 84 kwa kiwango cha lami ambayo nayo itakamilika mwezi ujao.

Barabara ya Masasi-Mangaka yenye urefu wa Km. 54 itajengwa kwa awamu tatu ambapo Km. 15 za lami zitagharimu shilingi bilioni 6.5 zitakapokamilika.

Rais pia amekagua Daraja la Umoja linalogharimiwa kwa ubia kati ya Tanzania na Msumbiji ambapo tayari asilimia 58 ya ujenzi wake umekamilika na mradi mzima utakamilika mwishoni mwa mwaka ujao.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments