Rais Kuhutubia siku ya ukimwi
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Rais Kuhutubia siku ya ukimwi
Rais Kuhutubia siku ya ukimwi
By Mike Mushi | Published  12/4/2007 | Habari Mpya | Rating:
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete atakuwa  mgeni rasmi katika maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ukimwi Duniani yatakayofanyika mkoani Tabora kesho (1 Desemba, 2007) na pia kutumia siku hiyo kuzungumza na wananchi kama ilivyo ada kwa Rais kuzungumza na wananchi kila mwisho wa mwezi.
 
Rais Kikwete amekuwa mstari wa mbele na mfano bora kwa wananchi wa Tanzania na dunia kwa ujumla kwa kuongoza katika upimaji yeye na mkewe, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kupima kwa hiari hapa Tanzania tarehe 14 Julai, 2007, kampeni ambayo imeendelea na kuongeza ujasiri kwa wananchi wa Tanzania ambapo siku ya kesho pia itatumika kuonyesha tathmini  na mafanikio ya kampeni aliyozindua Rais.
 
Na mfano huo unakwenda sambamba na kauli mbiu ya mwaka huu isemayo Zuia Ukimwi,Timiza Ahadi yako Ongoza mapambano, kauli inayotoa msisitizo kwa viongozi katika ngazi mbalimbali kuwa mfano kwa kuongoza mapambano dhidi ya Ukimwi.
 
Kauli mbiu hii pia inahimiza utekelezaji wa dhati wa malengo ya maendeleo ya Milenia (Millenium Development Goals) na maazimio yaliyowekwa kwenye mkutano maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ukimwi uliofanyika mwaka 2001 mjini New York Marekani.
 
Maazimio haya yaliridhiwa na nchi wanachama 189 wa Umoja wa Mataifa ikiwemo Tanzania, ambapo nchi zinatakiwa kutekeleza maazimio yaliyowekwa ifikapo mwaka 2015, likiwemo azimio la kupunguza maambukizi kwa asilimia 25 katika nchi zilizoathirika zaidi na ugonjwa huo.
 
Maadhimisho ya siku hii hutoa fursa kwa nchi na watu kutathmini hali halisi ya mwelekeo wa udhibiti na pia kubaini changamoto, mafanikio na kuweka mikakati ya baadaye ya kudhibiti janga la ukimwi.
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments