Mama Lowassa azindua albamu, achangisha sh. milioni 14.9/-
Guestbook
Tanzania, is a country on the east coast of east Africa.
 
JakayaKikwete.com
 »  Home  »  Habari Mpya  »  Mama Lowassa azindua albamu, achangisha sh. milioni 14.9/-
Mama Lowassa azindua albamu, achangisha sh. milioni 14.9/-
By Irene K. Bwire | Published  12/16/2007 | Habari Mpya | Rating:
 MKE wa Waziri Mkuu, Mama Regina Lowassa leo (Jumapili, Desemba 16, 2007) amezindua albamu ya nyimbo za dini na kuchangisha sh. milioni 14.9 katika mnada wa kanda na CD za kwaya ya Mt. Don Bosco.
 
Mama Lowassa alizindua mnada wa kuuza kanda (audio tapes) mbili na CD mbili za mwanzo kwa sh. milioni 7.6 ambapo kati ya hizo, sh. milioni 4 zilitolewa na Bw. Joseph Tango ambaye ni mlezi wa Kwaya na sh. 3.6 zilitolewa na Bw. Anderson aliyekuwa akichuana na Bw. Tango.
 
Katika mnada huo, picha ya mama Lowassa ilinunuliwa kwa sh. milioni moja na Bw. Nolaskus Mpota ambaye baadaye alimkabidhi mgeni rasmi kama zawadi.
 
Akizungumza katika uzinduzi wa albamu hiyo iitwayo ‘majibu’ uliofanyika kwenye viwanja vya parokia ya Kristu Mfalme Tabata, Mama Regina Lowassa aliwataka wazazi kuwahimiza vijana washiriki kwenye kwaya kwani mbali ya kumtumikia Mungu pia wanapunguza nafasi za vishawishi na ushiriki wa vitendo hatarishi.
 
“Nawaomba wazazi wenzangu wahimizeni vijana wengine washiriki katika kazi za kanisa… huko wataweza kujijenga kiroho na kupata majibu ya kumfurahisha Mungu; yapo maeneo mengi ambayo tukiwaelekeza wataweza kuwa vijana wazuri wa kutegemewa na jamii.”
 
Mama Lowassa alionya kwamba vijana hawana budi kufundishwa wayashike mafundisho ya Kanisa na kuepuka vitendo vyote viovu. “Wasipoelekezwa na wakiachwa watangetange watapata nafasi ya kushiriki mambo ambayo ni machukizo mbele ya Mungu na aibu mbele ya jamii,” alisema.
 
Alimwomba Paroko wa Tabata, Padre Cyprian Karugaba, kwa kushirikiana na mlezi wa Kwaya na Mwenyekiti wa Kwaya, Bw. Deo Bantulaki watafute siku maalum ya kukutana naye na kupanga sikuu maalum kwa ajili ya harambee. Alifikia uamuzi huo baada ya kuelezwa katika risala yao kwamba wanahitaji sh. milioni 23 kwa ajili ya kuendesha miradi ya ushonaji, upambaji, upishi, kuunga vyuma na useremala, hudma kiofisi (secretarial services) na kuanzisha kituo cha elimu.
 
Katika risala iliyosoma na katibu wa kwaya, Bi. Restituta Kifaru, wanakwaya hao walisema wamepata eneo la ekari 10 huko Chanika ambalo linahitaji kununuliwa kwa sh. milioni 10 na kwamba wanatarajia kulitumia kuanzisha kituo cha elimu.
 
Bi Kifaru alisema miradi yote hiyo ikianza, inatarajiwa kutoa ajira kwa wanakwaya 30 na vijana wengine 10 ambao si wanakwaya.
 
How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent

Verification:
Enter the security code shown below:
img


Add comment
Comments