WAZIRI MKUU Edward Lowassa
amesema Serikali imetoa jumla ya sh. bilioni 13 ili kuwalipa wakandarasi wote
nchini ambao walikuwa na madai kwa vipindi mbalimbali.
SERIKALI itayaendeleza mazuri yote yaliyonzishwa na aliyekuwa mbunge wa Kiteto, Benedict Losurutia ili kumuenzi mbunge huyo ambaye wakati wa uhai wake alipania kuwaendeleza wananchi wa Kiteto.
MAKAMU WA RAIS wa Cuba, Bw. Esteban Lazo Hernandez amesema jambo kubwa ambalo limemgusa na anaondoka nalo kutoka Tanzania ni jitihada ya Watanzania kupambana na maisha.
MKE wa Waziri Mkuu, Mama Regina Lowassa leo (Jumapili, Desemba 16, 2007) amezindua albamu ya nyimbo za dini na kuchangisha sh. milioni 14.9 katika mnada wa kanda na CD za kwaya ya Mt. Don Bosco.
Rais Jakaya Kikwete amewahakikishia wananchi wa wilaya ya Mafia kwamba, Serikali itamfuatilia na kumbana mkandarasi aliyepewa kazi ya kukarabati na kupanua njia ya kurukia na kutua ndege katika uwanja wa ndege wa Mafia.